RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein |
ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amesema kuanzia mwezi Julai mwaka
2019,Zanzibar haitakuwa tena na tatizo la uhaba wa dawa kwa magonjwa yote
yanayowakabilia wananchi wake.
Dk.Shein amebainisha hatua hiyo
katika uwanja mpira shule ya Michenzani mara baada ya kukifungua kituo kipya
cha afya cha Michenzani wilaya ya Mkoani ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema hilo linawezekana kutokana
na uchumi wa Zanzibar kuimarika hatua kwa hatua ambapo wananchi wa Zanzibar
wataondokana na shida waliyonayo hivi sasa kutokana na uhaba wa dawa uliopo
kwenye vituo vya afya pamoja na hospitali kadhaa.
Katika hatua nyengine Dk.Shein amewataka
wananchi wa Michenzani na vijiji jirani kuhakikisha wanakilinda na kukienzi
kituo hicho cha afya.
Chanzo:Zanzibar24
No comments:
Post a Comment