Monday, 15 January 2018

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi Mh Raphael Kalinga amesema tayari ametoa taarifa kwa katibu mkuu kuarifu kuhusu Kata ya Katumba katika halmashauri hiyokutokuwa na Diwani tangu mwaka jana.

Demokrasia na maendeleo Chadema Mh Rhoda Kunchela


NSIMBO

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi Mh Raphael Kalinga amesema tayari ametoa taarifa kwa katibu mkuu kuarifu kuhusu Kata ya Katumba katika halmashauri hiyokutokuwa na Diwani tangu mwaka jana.

Akizungumza na Mpanda radio fm mapema leo kupitia kipindi cha Kumekucha Tanzania Karinga amesema halmashauri inajipanga kwenda katika kata hiyo ili kukutana na watendaji wakiwemo wananchi ili waendelee kutoa ushirikiano kwa diwani wa viti maalumu.

Katika hatua nyingine amesema wanasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu kujua hatima ya suala hilo.

Mapema siku ya jana Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mh Rhoda Kunchela amesema kitendo cha wananchi wa kata hiyo kukosa Diwani hakikubaliki kwani kinadhoofisha jitihada za maendeleo  ya wananchi.

Diwani wa kata hiyo Seneta Baraka alifungwa mwaka jana miaka 3 jera  kwa kosa la kupokea rushwa kwa mfugaji wa kata hiyo ili amuidhinishie eneo la kufugia ambalo limepigwa marufuku na Mahakama.


Chanzo:Paul Matius

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...