Morogoro Tanzania |
Morogoro.
Baraza
la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Morogoro limemnyang'anya mwekezaji ekari 389 za
ardhi na kuzirejesha kwa serikali ya Kijiji cha Melela kwaajili ya matumizi ya
wananchi.
Akisoma
uamuzi huo ,Mwenyekiti wa Baraza hilo Prosper Makwandi amesema baraza limeridhishwa
na ushahidi uliowasilishwa mahakamani na wadaiwa ambao ni Halmashauri ya Kijiji
Melela wilayani Mvomero.
Shauri
hilo la madai namba 69 lilifunguliwa mwaka 2012 na mdai Kizota Wacha
akiiilalamikia Halmashauri ya kijiji cha Melela kumpora eneo la ardhi lenye
ukubwa wa ekari 504 ambazo alirithi toka kwa baba yake Wacha Rombo.
Katika
utetezi wake Mdai (Wacha) ambaye alikuwa akiwakilishwa na Wakili Mariam Kapama
aliliambia baraza kuwa baba yake alipewa eneo hilo na halmashauri ya Kijiji cha
Melela mwaka 1992 hivyo anashangaa kuona kijiji kikitumia tena eneo hilo kwa
matumizi ya wanakijiji.
Halmashauri
ya Kijiji ambayo ilikuwa ikiwakilishwa na Wakili Alex Sikalumba imedai kuwa
eneo alilopewa baba yake mdai lilikuwa ni ekari 50 na baadaye aliongezewa 15 na
kufanya jumla ya ekari 65.
Mwenyekiti
wa Baraza hilo,Makwandi amesema baada ya baraza kusikiliza utetezi wa pande
zote mbili baraza liliridhia kwamba baba yake mdai (Wacha) alipewa ekari 50
awamu ya kwanza na kuongezewa ekari 15 na baadaye aliomba ekari 50 kama
alivyoeleza mdai hivyo kufanya jumla ya ekari 115.
“Hivyo
baada ya kuridhishwa na vielelezo vya pande zote baraza linaelekeza kuwa
mdai apewe ekari 115 ambazo alirithi toka kwa baba yake na ekari zilizobaki
zitaendelea kuwa mali ya halmashauri ya kijiji cha Melela” amesema
Mwenyekiti huyo.
Uamuzi
huo wa Baraza la ardhi umekuja wakati ambao Rais amebatilisha umiliki wa ekari
14,800 za mashamba ambayo wamiliki wake walishindwa kuyaendeleza katika wilaya
za Mvomero,Kilosa na Kilombero.
Hata
hivyo kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Mashariki Juliana Pilla
orodha ya mashambapori yaliyowasilishwa Wizara ya Ardhi kuomba kufutiwa umiliki
ni zaidi ya ekari 47,000.
No comments:
Post a Comment