Serikali
ya Brazil imefutilia mbali hifadhi kubwa ya taifa katika eneo la Amazon ili
kutoa fursa ya uchumbaji wa madini katika eneo hilo.
Hifadhi
hiyo, yenye ukubwa wa kilomita 46,000 mraba (maili mraba 17,800) hupatikana
katika majimbo ya kaskazini ya Amapa na Para na inaaminika kuwa na dhahabu
pamoja na madini mengine.
Serikali
imesema maeneo tisa ya uhifadhi na ardhi inayolindwa ya watu asilia, ambayo
yanapatikana ndani ya hifadhi hiyo, yataendelea kulingwa kisheria.
Lakini
wanaharakati wa hutetea uhifadhi wa utamaduni na mazingira wamelalamika kwamba
maeneo hayo yataathirika pakubwa.
Kwa
jumla, inakadiriwa kwamba 30% ya eneo lote la hifadhi hiyo litatumiwa kwa
uchimbaji wa madini.
Agizo
rasmi kutoka kwa Rais Michel Temer lilifutilia mbali hifadhi hiyo ambayo
hufahamika kama Hifadhi ya Taifa ya Shaba Nyekundu na Washirika (Renca).
MaurĂcio
Voivodic, mkuu wa shirika la uhifadhi wa wanyama la WWF nchini Brazil,
alitahadharisha mwezi jana kwamba uchimbaji wa madini katika eneo hilo
utasababisha "ongezeko kubwa la watu, ukataji mkubwa wa miti, kuharibiwa
kwa
No comments:
Post a Comment