Mkuu wa wilaya ya Tanganyika bwana salehe Mhando |
Tanganyika
Wilaya ya
Tanganyika Mkoani Katavi imejipanga kuinua mazao ya biashara ili kuweza
kuongeza mapato na kuinua uchumi wa wananchi.
Ameyasema
hayo mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe Mhando wakati akizungumza na
mpanda redio na kusema kuwa kwa sasa wamejipanga kuinua mazao mbadala kama
karanga ,alizeti na pamba kwa lengo la kuongeza kipato kwa halmashauri na
wananchi kwa ujumla.
Aidha
amebainisha kwasasa wanajipanga kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kulima
katika ubora na kuzalisha pamba bora ambazo zitapata soko ndani ya nchi na hata
nje ya nchi
hata hivyo
amesema wananchi wajitokeze kujiandikisha wale ambao watakuwa tayari kulima
pamba ili waweze kupewa pembejeo kama mbegu na madawa.
Mhando
amewataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kuzalisha pamba na
kujiongezea kipato ambacho kitawawezesha kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment