Monday, 15 January 2018

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka Hospitali na vituo vya Afya nchini kuhakikisha wagonjwa hawauziwi damu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu


DAR ES SALAAM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka Hospitali na vituo vya Afya nchini kuhakikisha wagonjwa hawauziwi damu.

Ummy amesema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu ambayo inafanywa na Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini jijini Dar es salaam.

Aidha Waziri Ummy amewataka viongozi wa Hospitali na vituo vya Afya vya Serikali wahakikishe kuwa wanaweka matangazo yanayoelimisha wananchi kuwa damu haiuzwi bali inatolewa bila ya malipo na matangazo yaelekeze wananchi sehemu ya kutoa malalamiko.

Waziri Ummy amewaasa wananchi hasa wanaume kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili kuweka akiba ya kutosha katika benki ya damu hatimaye kupunguza uhaba wa damu katika benki ya damu na kuokoa vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu.


Chanzo:Eatv

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...