Monday, 15 January 2018

Watu 1,500 wamehamishwa kutoka visiwa vya Papua New Guinea, kutokana na mlipuko wa volcano.


Port Mores

Watu 1,500 wamehamishwa kutoka visiwa vya Papua New Guinea, kutokana na mlipuko wa volcano.

Volkano katika kisiwa cha Kodovar ilianza kutoa moshi na majivu wiki iliyopita, na kusababisha kuhamishwa kwa zaidi ya watu 500 kwenda kisiwa kilicho karibu cha Blup Blup.

Baada ya mlipuko kuzidi sasa wale waliokimbilia kisiwa cha Kodovar sasa watahamishiwa kwingine.

Papua New Guinea ni nyumbani kwa milima kadhaa ya volkano.Walioshuhudia huko Blup Blup kusini mwa kisiwa cha Kadovar waliripoti mlipuko mkubwa kutoka kwa volkano siku ya Ijumaa na moto mkubwa ukitoka kwenye mlima huo.

Wanasayansi baadaye waligundua viwango vikubwa vya gesi ya sulphur dioxide kutoka na volkano hiyo.

Chanzo :Alinanuswe Edward


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...