IRINGA.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard
Kasesela amepiga marufuku vitendo vya wanaume walio kwenye ndoa kupiga wake
zao, akisema atakayebainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa
kampeni ya ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari Tagamenda wilayani Iringa
amefafanua kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na baadhi ya familia kuchukulia
vitendo hivyo kuwa ni vya kawaida.
Ameeleza kuwa hadi sasa
ameshawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wanaume watatu na kuwataka
wanawake wanaopatwa na masaibu hayo kutoa taarifa kwake ili achukue hatua
badala ya kuona kuwa vitendo hivyo ni sehemu ya maisha yao.
Aidha amebainisha kuwa hakuna
mafanikio yanayoweza kupatikana katika familia endapo mama na baba wanaingia
katika ugomvi na hata kuumizana.
Hatua ya Kasesela kuwataka wanawake
kutoa taarifa kwa vitendo vya ukatili ikiwemo vipigo imepokelewa kwa furaha na wanawake waliohudhuria mkutano
huo ambao wamesema itasaidia kurejesha heshima na utu.
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment