Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi kupitia Chadema Rhoda Kunchela |
KATAVI
Mbunge wa viti maalumu
mkoa wa Katavi kupitia Chadema Rhoda
Kunchela amesema kitendo cha kata ya
katumba halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kutokuwa na diwani ni kuchelewesha
maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo.
Hayo yamebainishwa leo
na Mbunge huyo wakati akizungumza na Mpanda Radio na kusema kuwa wananchi
wanakosa uwakilishi na kushauri uchaguzi
ufanyike ili apatakane diwani mwingine .
Diwani aliyekuwa
akiongoza kata hiyo Mh Seneta Baraka amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela
tangu mwaka uliopita kwa kosa la kupokea
rushwa.
Katika hatua nyingine
Mh Kunchela amezungumzia ziara
aliyoifanya mwenyekiti wa Bawacha taifa
Halima Mdee amabye pia ni mbunge wa jimbo la kawe na kusema ziara hiyo imefanyika mkoani katavi ikilenga
kuimarisha uhai wa chama hicho.
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment