Sunday, 14 January 2018

Kiongozi mpya wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC, Cyril Ramaphosa ametoa mwito wa kuzikabili hitilafu zinazoathiri utendaji kazi wa chama hicho na pia ametaka kuwepo umoja katika ngazi zote za chama.

Cyril Ramaphosa

JOHANASBAG

Kiongozi mpya wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC, Cyril Ramaphosa ametoa mwito wa kuzikabili hitilafu zinazoathiri utendaji kazi wa chama hicho na pia ametaka kuwepo umoja katika ngazi zote za chama.

Ramaphosa alitoa mwito huo alipohutubia kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini East London nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuadhimisha mwaka wa106 tangu kuundwa kwa chama cha ANC.

 Kiongozi huyo wa ANC amesema chama hicho kimegawanyika vibaya kutokana na upendeleo na ufisadi.

Hata hivyo Rhamaphosa aliyechaguliwa mwezi uliopita kuchukua nafasi ya rais Jacob Zuma, hakuzungumzia juu ya miito ya watu wanaotaka rais Zuma aondolewe madarakani mara moja.

 Muhula wa rais huyo utamalizika mwaka ujao baada ya kufanyika uchaguzi.

Chanzo:CRI

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...