Spika wa Bunge la Tanzania Mh. Job Ndugai |
DODOMA
Spika wa Bunge Job Ndugai ameiagiza Kamati ya
Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujadili na kuchunguza kauli ya Mkuu wa Mkoa
wa Njombe Christopher Ole Sendeka inayodaiwa kudhalilisha bunge.
Hatua
hizo za Mh. Spika zimekuja baada ya kauli zinazodhaniwa kuwa ni za Mh.
Olesendeka zikiashiria kejeli na dharau kwa Bunge ambazo zilikuwa zikitamkwa
kwa Lugha ya Kimasai, kiswahili na Kingereza.
Taarifa
iliyotolewa kwa wanahabari imesema kwamba , Spika ameelekeza kuwa Kamati hiyo
imuite na kumhoji Kiongozi huyo ikiwa ni pamoja na kuchunguza
ukweli na dhamira ya kauli hizo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa
kuchukuliwa na Bunge.
Kauli
zinazodaiwa kuwa ni za Ole- Sendeka zilisikika zikisema kwa bunge
limemomonyolewa.
Chanzo:Etv
No comments:
Post a Comment