Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe |
DAR ES SALAAM
Siku moja baada ya Waziri mkuu mstaafu wa
Tanzania Edward Lowasa ambaye 2015 aligombea urais kupitia Chadema kutoa kauli ya Kukubaliana na utendaji wa
Rais Dk John Pombe Magufuli chama hicho
kimasema huo sio msimamo wake.
Hayo yamesemawa na Mwenyekiti wa chama cha
demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe na kueeleza kuwa chama hicho
hakiwezi kuwa na kauli zinazo pingana na uhalisia.
Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowasa na Rais Dk John Pombe Magufuli jana wakiwa ikulu |
Hapo Jana Waziri mkuu huyo wa zamani akiwa ikulu Jijini Dar es salaam amemwagia sifa rais John Pombe Magufuli kuwa mchapakazi akiweka bayana baadhi ya mambo kuwa ni utekelezaji wa elimu bure sanjari na uimarishaji wa miundo mbinu.
Chama cha demokrasia na maendeleo chadema
kimekuwa mkosoaji mkuu wa serikali hasa katika kile kinachodaiwa kuwa ni kuwepo
kwa mtikisiko wa demokrasia nchini.
Chanzo: Etv
No comments:
Post a Comment