Wednesday, 10 January 2018

Mawaziri wa serikali za nchi za Afrika wamesisitiza haja ya kukabiliana na suala la uhamiaji kwa njia shirikishi.

Waziri wa mahusiano ya kimataifa na ushirikiano wa Afrika Kusini Bibi Maite Nkoana-Mashahane


RABAT

Mawaziri wa serikali za nchi za Afrika wamesisitiza haja ya kukabiliana na suala la uhamiaji kwa njia shirikishi.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Morocco Bw. Nasser Bourita amesema, ajenda ya Afrika kuhusu suala la uhamiaji italifanya suala la uhamiaji liwe kichocheo cha maendeleo ya ushirikiano, nguzo ya ushirikiano wa kusini na mwelekeo wa kuhimiza mshikamano.

Waziri wa mahusiano ya kimataifa na ushirikiano wa Afrika Kusini Bibi Maite Nkoana-Mashahane, amesema kama suala la uhamiaji litashughulikiwa vizuri, litaleta fursa nyingi kwa Afrika.


Chanzo:Cri swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...