Wednesday, 10 January 2018
Wapiganaji zaidi ya 107 wa kundi la Boko Haram wameuawa katika operesheni ya jeshi la Nigeria.
ABUJA
Wapiganaji zaidi ya 107 wa kundi la Boko Haram
wameuawa katika operesheni ya jeshi la Nigeria, miongoni mwao zaidi ya 50
wameuawa karibu na ziwa Chad na wengine zaidi ya 57 wameuawa kwenye eneo la
Metele la jimbo la Borno nchini Nigeria.
Msemaji wa jeshi la Nigeria Bw. Sani Usman
ametoa taarifa akisema lengo la operesheni hiyo ni kuondoa wapiganaji wa kundi
hilo waliosalia katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji huyo ameongeza kwamba askari wanne wa
jeshi la Nigeria na raia mmoja anayejitolea pia wameuawa kwenye operesheni
hiyo, baada ya deraya walilokuwa wakisafiria kugongwa na gari lenye mabomu ya
kienyeji lililoendeshwa na wapiganaji wa kundi hilo.
CHANZO: DW SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...
-
Kabale, Uganda. Mpinzani mkuu wa Uganda na kiongozi wa Forum for Democratic Change (FDC) Dk Kizza Besigye amekamatwa. ...
-
KIGOMA . VITUO vya afya Uvinza na Nguruka vilivyopo wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo yaup...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...

No comments:
Post a Comment