NSIMBO
Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi
inatarajia kufanya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani katika kata ya
Itenka.
Taariiifa hiyo imetolewa na afisa habari wa
halimashauri ya Nsimbo John Mganga wakati
akizungumza na mpanda radio kwa njia ya simu ambapo ameeleza kuwa nia ni
kuihamasisha jamii kujua nafasi ya mwanamke katika maendeleo ya uchumi nchini.
Aidha amesema kuwa maadhimisho hayo yatakuwa
yakifanyika katika kata mbalimbali za halimashauri hiyo kila mwaka.
Maadhimisho ya mwanamke duniani hufanyika
kila mwaka tarehe 08 mwezi wa tatu ambapo
mwaka huu yakiwa na kauli mbiu isemayo“kuelekea uchumi wa viwanda kuimarisha
usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wanawake vijijini”.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment