MPANDA
Wananchi
wametakiwa kuzingatia ujenzi wa majengo ya makazi yao kwa kufuata ushauri wa
jeshi la zima moto na uokoaji ili kurahisiha huduma pindi majanga ya moto
yanapojitokeza.
Hayo
yamesemwa na Afisa polisi kitengo cha ukaguzi
Wilfred Luhega wakati akizungumza na mpanda radio na kueleza kuwa tatizo
la makazi yasiyokuwa na mpangilio pamoja na uchimbaji holela wa visima ni
changamoto kubwa na wakati mwingine kusababisha vifo .
Aidha
ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika ofisi zao kwaajili ya kupata elimu ya zimamoto na uokoaji ili kuweza kusaidia
kupunguza majanga yasiyokua ya lazima.
Mara
kadhaa Maafisa wa Jeshi la zimamoto na
uokoaji nchini wamekuwa wakilalamikia
ukosefu wa vitendea kazi kama kikwazo cha kukwamisha utendaji kazi.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment