Maegesho ya bajaji city centre |
Mwenyekiti wa pikipiki za
miguu mitatu maarufu kama bajaji wa
halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Rashidi Juma amewataka madereva
wa bajaji kuendelea kutoa tozo ili kuweza kupata usajili wa namba za maegesho.
Ameyasema hayo alipozungumza
na mpanda radio na kusema kufanya hivyo itawasaidia madereva kuepuka usumbufu
wa kukosa maegesho huku akitolea ufafanuzi suala la bajaji kupewa mihuri na
namba na nyingine kupewa mihuri bila namba.
Kwa upande wa madereva wamekuwa
na maoni tofauti kuhusu kuwepo kwa tozo hizo.
Ofisa Mfawidhi wa Sumatra
Mkoani Katavi Amani Mwakalebela amesema kuwa kutowepo kwa namba katika bajaji
hizo ni kutokana na baadhi ya madereva kutokutimiza masharti yanayotakiwa.
Zoezi la ugawaji wa namba za
maegesho limefanyika kutokana na uwepo wa matukio ya uharifu na uporaji ambayo yanaendelea
kutokea mkoani hapa.
Chanzo:Furaha Kimondo
No comments:
Post a Comment