Mbunge wa Mpanda vijini Mh. Suleiman Kakoso |
Mbunge wa Mpanda vijini Suleiman Kakoso ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
TAKUKURU mkoani hapa kufuatilia ili
kuondoa ubadhilifu wa fedha katika miradi mikubwa ya serikali .
Ameyazungumza hayo katika kikao cha 11 cha kamati ya ushauri mkoa wa Katavi
na kusema kuwa fedha nyingi za miradi ya serikali zimekuwa zikifanyiwa ubadhilifu na kuiomba
taasisi hiyo kufuatilia kwa karibu ili kuweza kulinda fedha hizo.
Akijibu swali la mbunge huyo Mkuu wa Takukuru Mkoa wa
Katavi, "kutokana na changamoto za fedha na
raslimali watu imekuwa ikisababisha kupunguza kasi ya kukamilika kwa uchunguzi
wa matukio ya rushwa ambayo taasisi hiyo imekua ikifuatilia
"amesema John Minyenya
"amesema John Minyenya
Aidha ametoa wito kwa wabunge na viongozi wa ngazi zote kutoa ushirikiano
pindi waonapo dalili za ubadhilifu wa fedha katika miradi mbalimbali.
Miradi mingi ya maendeleo mkoani katavi imekuwa ikisua sua katika
ukamilishwaji huku ikielezwa kuwa chanzo ni ubadhilifu wa fedha.
Chanzo:RESTUTA NYONDO
No comments:
Post a Comment