Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga
Watumishi
wa umma katika Mkoa wa Katavi wameombwa kutoa ushirikiano kwa kamati maalumu
iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ili kubaini wafanyakazi hewa katika
ofisi za umma.
Watumishi wa umma katika Mkoa wa Katavi wakiwakatika ukumbini katika kamati maalumu ya kubaini wafanyakazi hewa katika ofisi za umma. |
Wito
huo umetolewa katika kikao cha mapendekezo ya sekretarieti ya bajeti ya Mkoa wa Katavi uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ambapo Mkuu wa mkoa alikuwa akizungumza na wafanyakazi wa hao .
Aidha
Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa wafanyakazi katika halmashauri zote kuhamia
katika vituo vyao vyote vya kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa
wananchi
Watumishi wa umma katika Mkoa wa Katavi wakiwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga |
Katika
kipindi cha mwaka 2018/2019 mkoa wa katavi umepanga kutumia shilingi bilioni
mia moja kumi na tisa namilioni mia moja na mbili na laki sita sitini na tatu
elfu na mia tatu na nne(119,102,663na 304) sawa na asilimia 35% kwaajili ya
utekelezaji mbalimbali wa miradi ya maendeleo.
Chanzo:Paul
Mathias
No comments:
Post a Comment