Wanafunzi wa
shule ya Msingi Kabungu iliyoko kata ya
kabungu Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wameiomba serikali kuwaboreshea
madarasa ambayo yaliezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.
Wameyasema
hayo walipozungumza na mpanda radio shuleni hapo " kuezuliwa kwa madarasa kumetuathiri kwani vipindi vingi vimepunguzwa hali
inayopelekea baadhi ya vipindi kutofundishwa pia madaftari na vitabu vingi vimeharibika ",walisema wanafunzi hao.
Kwa upande
wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema kuwa upepo huo umesababisha uharibifu
wa vitabu na madaftari yaliyokuwepo katika maktaba na kuiomba halmashauri
kuwasaidia kufanya marekebisho ya miundombinu ili kuboresha elimu.
Ili kuongeza
ufaulu kwa wanafunzi inatakiwa miundominu iwe imara inayoweza kuwa rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu.
No comments:
Post a Comment