KATAVI
Imeelezwa kuwa changamoto ya Miundombinu
ikiwemo Bara bara imekuwa ni kikwazo kwa wananchi na watalii kushindwa kutembea
hifadhi za ndani ikiwemo ya hifadhi ya Katavi.
Katika mazungumzo maalum na Mpanda redio mmoja
ya watumishi katika hifadhi hiyo Private Ezekiel eliufoo amesema endapo maboresho yatafanywa katika
Nyanja hizo yatasaidia kukuza utalii wa
ndani.
Aidha Katika hatua nyingine amebainisha pia
ujangili ukiwemo wa tembo umepelekea changamoto katika hifadhi hiyo inayopoteza
tembeo wengi.
Awali Daudi Godowin ambaye ni afsa utalii
ndani ya hifadhi hiyo amewataka wananchi wakiwemo wa katavi kujiwekea taratibu
za kutembelea hifadho kuweza kujifunza masuala mbalimbali.
Hifadhi ya Katavi ni hifadhi ya tatu kwa
ukubwa kati ya hifadhi kumi na sita zilizopo nchini Tanzania na ambayo pia
imekuwa ikifanya kazi ya kuhifadhi mazingira ,kuifadhi vyanzo vya maji na
wanyama.
Chanzo:Furaha Kimondo
No comments:
Post a Comment