MLELE
Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi Mkoani Katavi Beda Alfred amewataka viongozi wa ngazi zote katika
kata kutekeleza majukumu yao.
Akiwa ziarani wilayani Mlele
katika kata ya utende wakati akizungumza na Wajumbe hao amesema kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi kutawasaidia kuwaweka karibu na wananchi wao.
Kwa upande wao wajumbe hao
wamesema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana na ni pamoja na migogoro ya
ardhi baiba ya wakulima na wafugaji na vitendea kazi.
Katika ziara hiyo wilayani mlele
Mwenyekiti wa ccm mkoa ametembelea pia mradi wa umeme uliopo katika kijiji cha
Uzega.
Chanzo:Furaha Kimondo
No comments:
Post a Comment