Monday, 26 February 2018

WAKAZI WA KATA YA NSEMULWA WAMEASWA KUCHANGIA KWA WINGI KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA.

Picha ya kituo cha afya 

MPANDA
Wakazi wa Kata ya Nsemulwa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameaswa kuchangia kwa wingi asilimia ishirini kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.
Wito huo umetolewa na diwani wa kata hiyo Mh.Bakari Kapona wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mikakati ya ujenzi wa kituo cha huduma ya afya ili kutatua kero ya wananchi kupata matibabu umbali mrefu.
Aidha Mh. Kapona amesema "Manispaa ya Mpanda imetenga shilingi milioni 35 kwa ajili ya kituo hicho na kinachosubiriwa kwa sasa ni wananchi kuchangia nguvu zao ambapo ujenzi wa unatarajiwa kuanza fikapo mwezi juni Mwaka huu".
Kata ya Nsemulwa yenye wakazi wapatao elfu kumi na moja ni miongoni mwa kata 15 za Manispaa ya Mpanda na wakazi wake kwa sasa wanapata huduma ya afya katika vituo vilivyo jirani au kulazimika kwenda Hospitali ya wilaya Mpanda.
Chanzo:Issack Gerald

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...