MPANDA
Wananchi wilayani mpanda mkoani katavi wamelalamikia ubovu wa baadhi
ya barabara katika maeneo yao chanzo
kinachopelekea ukosefu wa huduma za
kijamii kwa wakati.
Wamesema hayo wakizungumza na mpanda redio huku wakibainisha adha
wanayoipata kutokana na changamoto ya
barabara hizo.
Kwa mujibu wa kaimu mratibu wa
tarura mkoa mhandisi zuberi kirenza ametaja barabara zilizoko kwenye mpango wa
kutengenezwa kwa mwaka huu.
Aidha barabara zitakozotengenezwa mpanda mjini zitagharimu kiasi cha
shilingi milioni 360 huku barabara za
mjini zikigharimu shilingi milioni165 na vijijini milioni 195.
No comments:
Post a Comment