MPANDA
Jeshi la Polisi Mkoani
Katavi linamsaka mkazi wa Airtel ya kwamkumbo kwa tuhuma za kumjeruhi vibaya kwa
kumchoma moto mwanae aitwaye Nohadia
Michael kwa kumtuhumu kuiba kiasi cha shilingi mia tano.
Katibu wa dawati la
jinsia mkoani katavi Koplo Judithi Mbukwa
Ameimbia Mpanda redio kuwa Tukio hilo limetokea tarehe February 23 mwaka huu katika manispaa ya mpanda ambapo mzazi huyo
alimchoma viganja vya mkono kwa moto wa jiko la mkaa Mwanaye na kumsababishia maumivu makali.
Aidha Coplo
Mbukwa ametoa wito kwa wananchi na
kuacha kutumia hasira katik kufanya maamuzi mbalimbali
Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii Manipsaa ya
Mpanda Bi, Agnes bulaganya ametoa wito,amesema wanaendelea
kumtibu motto huyo mpaka atakapopona na kuitaka jamiii kuacha vitendo hivyo vya ukatili wa dhidi ya
watoto ikiwemo
Kumjengea mazingira salama dhidi ya vitendo vya
ukatili kwa na utetezi wa kutumia mifumo sahihi ya ulinzi mtoto.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 ni waraka
unaoshughulikia masuala ya kitaifa yanayohusu haki na ulinzi wa mtoto
inaainisha kuwa Suala la ulinzi wa
mtoto ni jukumu la jamii nzima, mlezi na mzazi mmoja mmoja kwa nafasi yake
katika ngazi ya familia pamoja na serikali kwa ujumla.
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment