Thursday, 15 February 2018

Mkazi wa matandalani kijii cha sango anayefahamika kwa jina la Wiliam Piu,amefikishwa mahakamani kwa kosa la kukamatwa na meno ya tembo


MPANDA
Mkazi wa matandalani  kijii cha  sango anayefahamika kwa jina la Wiliam Piu,amefikishwa mahakamani kwa kosa la kukamatwa na meno ya tembo.

Tukio hilo limetokea tarehe 26 mwezi wa kwanza saa 10 jioni katika kijiji cha sango ambapo mshitakiwa huyo mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa matandalani amekamatwa na vipande 4 vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola za kimarekani 15000 ambayo nisawa na  shilingi za kitanzania  34,050,000 ambayo ni mali ya serikali kinyume na ruhusa kutoka kwa msimamizi wa  wanyamapori .

Kesi hiyo imesikilizwa jana katika mahakama ya wilaya ya mpanda  mbele ya hakimu Chiganga Tengwa na wakili wa serikali Flaviana Shiyo na mtuhumiwa hakutakiwa kuongea chochote.


Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 19 mwezi huu hukumtuhumiwa akirudishwa rumande na kusubiri kusomewa shitaka lake tena.
Chanzo:Furaha Kimondo

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...