Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako |
KAGERA
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameahidi Sh50 milioni kwa ajili ya ujenzi
wa maabara ya shule ya sekondari ya kata ya Rulanda wilaya ya Muleba mkoani
Kagera iliyopewa jina lake.
Huku akimpongeza Rais John
Magufuli kupendekeza shule hiyo kuitwa Joyce Ndalichako, waziri huyo ameahidi
kutoa fedha hizo alipoitembelea shule hiyo na kuongeza Sh3milioni kwa ajili ya
kununua vitabu vya wanafunzi.
Amesema pamoja na ujenzi wa
barabara atashirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Muleba kuhakikisha
zinapatikana samani za kutosheleza shule hiyo, pamoja na huduma ya maji huku
akiwaomba wananchi kuendelea kuchangia upatikanaji wa maji.
Mkuu wa shule hiyo, Paul
Morigo amesema katika awamu ya kwanza ujenzi wa shule
hiyo ulianzishwa na wananchi kwa kuchangia vitu mbalimbali vyenye thamani
ya Sh 67.76 milioni .
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment