TANGANYIKA
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Salehe Mhando amesema hata
vumilia kufukuzwa kwa wanafunzi kwa ajili ya michango ya shule
Katika mazungumzo yaliyofanywa na Mpanda Redio ambapo ameeleza kuwa kitendo hicho licha ya kupingana na agizo la serikali lakini pia kinamuathiri mwanafunzi kisaikolojia.
Ametoa ufafanuzi kuwa michango ambayo inaendelea katika wilaya hiyo ni
ile ambayo inaendeshwa na wazazi wenyewe kama vile chakula kwa wanafunzi.
Katika hatua nyingine amewashukuru wananchi wa wilaya hiyo kuendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi
Chanzo:Alinanuswe Edward
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment