KATAVI
Wakulima wa zao la Tumbaku
wameiomba serikali kutekeleza ahadi ya kuwalipa marimbikizo yao ya fedha.
Hayo yamejiri baada ya agizo
lililotolewa na Naibu Waziri wa kilimo na mifugo dkt.Marry Mwanjelwa
alilowataka wakulima hao kulipwa fedha zao ndani ya siku saba.
Wakulima hao wameiomba serikali kubadilisha mfumo wa ulipaji wa fedha hizo kwani hawana elimu juu ya mfumo unaotimika ambao ni malipo ya dola za kimnarekani.
Naibu waziri alitoa agizo la kulipwa kwa fedha hizo ndani ya siku saba mnamo tarehe 2 feb katika bunge la 10 wakati akijibu swali la mbunge wa Nsimbo Richard Mbogo (CCM) aliyetaka kujua ni lini wakulima wa tumbaku mkoani Katavi watalipwa madeni yao ya zaidi ya dola za kimarekani laki nne wazodai vyama vya ushirika nchini.
Chanzo:Restuta Nyondo
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment