KATAVI
Wilaya ya mpanda mkoani Katavi inaongoza kwa matukio ya vifo vinavyotokana
na ajali za barabarani.
Taarifa hiyo imetolewa na kamanda wa polisi RPC mkoa wa
katavi Damas Nyanda katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
barabarani yaliyofanyika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili.
Kamanda Nyanda ameeleza vyanzo vya ajali hizo kuwa ni
ulevi,uzembe na ubovu wa miuondombinu
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpanda Liliani Matinga
amewataka wananchi kufanyia kazi elimu ambayo imekua ikitolewa na jeshi la polisi.
Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama nchini
yalizinduliwa mkoani kilimanjaro na Makamu wa Raisi mhe.Samia Suluhu
Hassani tarehe 16 october 2017 kauli
mbiu ikiwa ni “Zuia ajali,Tii sheria,Okoa maisha”.
CHANZO:RESTUTA NYONDO.
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment