DODOMA.
Vikosi vya ulinzi wa majini vya nchini Australia
vimekamata kilo 1,365 za dawa za kulevya aina ya heroine kipindi cha kati ya
Januari na Februari, kupitia bahari ya Hindi eneo la Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini
Dodoma, kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya
(DCEA), Rogers Sianga amesema kati ya kiasi hicho, kilo 965 zimekamatwa
Februari 2018 na kwamba,katia ya hizo 650 zilikuwa ziingizwe nchini.
Amesema mamlaka hiyo imekuwa ikivunja mitandao ya
dawa za kulevya na kwamba, kilo 200 zilikamatwa katika gari la Mtanzania
mpakani mwa Msumbiji na Afrika Kusini.
Kuhusu mbinu mpya ya watumiaji dawa za kulevya,
Sianga amesema baada ya dawa za kulevya kuanza kuadimika sasa wanatumia ugoro
na gundi.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment