DAR ES SALAAM.
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita) umesema kuanzia sasa ni
ruksa kutumia kitambulisho cha Taifa na cha kupigia kura kupata cheti cha
kuzaliwa.
Kaimu Ofisa Mtendaji, Emmy Husdon amesema wakati akitoa taarifa kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome wakati wa
ziara katika ofisi za wakala huo jijini Dar es Salaam.
Husdon amesema mafanikio katika mfumo wa usajili wa vizazi na vifo
kupitia mradi wa maboresho ya miundombinu ya Tehama (RCIP), ambao umetekelezwa
kwa majaribio mikoa ya Geita, Shinyanga na Dar es Salaam umekwisha kusajili
vizazi 6,794 na vifo 271.
Amesema katika usajili huo, mfumo umeweza kuunganishwa moja kwa moja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa (Nida).
SOURCE:MWANANCHI
#Chagia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment