Saturday, 10 February 2018

Chama cha waalimu Tanzania wilaya ya Mpanda mkoani katavi kimetoa jumla ya bati 100 kwa waalimu watano waliostaafu mwaka jana.



MPANDA

Chama cha waalimu Tanzania wilaya ya Mpanda  mkoani katavi kimetoa jumla ya  bati 100 kwa waalimu watano waliostaafu mwaka jana

Katibu wa Chama hicho mkoa wa katavi hamisi chinahova akikabidhi bati hizo  amesema hiyo ni  moja ya kuwaenzi na  kutambua kazi za waalimu kupitia chama hicho huku akiwasihi  kutumia na kuenzi zawadi hiyo kwa kuweka alama itakayowatambulisha mchango wa waalimu kwao.

Akizungumza kwa niaba ya wastaafu hao mwali  mery nkumbae amesema kupitia zawadi hiyo ya bati
kutawasaidia kuboresha maisha hao.

Awali Kabla Katibu wa CWT wilaya ya Mpanda mwalimu Wison masolwa  amesema Bati hizo 100  zenye jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja zimetolewa kwa wastaafu watano kwa kila mmoja bati 20 .

Chanzo:Paul Mathias
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...