Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Joseph Magufuli |
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John
Pombe Joseph Magufuli amewahakikishia mabalozi na wakuu wa mashirika ya
kimataifa waliopo hapa nchini kuwa katika kipindi cha mwaka 2018 serikali ya
awamu ya tano itaendeleza juhudi za kuendeleza mazingira ya uwekezaji.
Mh.Rais Magufuli amesema hayo katika halfa ya mwaka
mpya aliyowaandalia mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini hafla ambayo
imefanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu Jijini Dar es salaamu.
Katika hafla hiyo,rais ametoa wito kwa mabalozi hao
kuwahamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka katika nchi zao kuja
kuwekeza hapa nchini huku akisema serikali itatoa ushirikiano wote
utakaohitajika kwa wawekezaji watakaojitokeza.
Kwa upande wake naibu kiongozi wa mabalozi na wakuu
wa mashirika ya kimataifa hapa nchini ambaye ni balozi wa Saharawi Mh.Brahim
Salehe El-mami Buseif mbali na kumpongeza Rais Mh.Dkt.John Magufuli kwa uongozi
wake wakuu wa mashirika ya kimataifa wataendelea kushirikiana na serikali
katika kufanikisha mendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Chanzo:Tovuti
Ikulu ya Rais
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment