Monday, 5 February 2018

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ala kiapo bungeni leo.


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi akila kiapo cha uaminifu bungeni baada ya kuanza kwa kikao cha tano cha mkutano wa kumi wa Bunge, Mini Dodoma leo. 
Dodoma. 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Adelardus Kilangi amekula kiapo cha uaminifu bungeni, kukabidhiwa vitendea kazi na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Dk Kilangi ameapa leo Februari 5, 2018 kabla ya kuanza kwa kikao cha tano cha mkutano wa 11 wa Bunge, mjini Dodoma.
Mara baada ya kuapa, Dk Tulia alimkabidhi AG vitendea kazi hivyo.
Februari Mosi, 2018 Rais Magufuli alimteua Dk Kilangi kuwa AG mpya na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Pia, alimtea aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu.
Februari 3, 2018 wateule hao waliapishwa na Rais Magufuli Ikulu, Dar es Salaam na kueleza mikakati yao  katika majukumu yao mapya.
 Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...