Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Februari, 2018 amempandisha cheo na kumteua Bw. Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa Rais Dkt. Magufuli amempandisha cheo Bw. Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Kwa taarifa kamili soma hapa chini.
Chanzo:Eatv
#CHangia Damu Okoa Taifa
Chanzo:Eatv
#CHangia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment