Thursday, 8 February 2018

Ruksa kadi ya kupiga kura kupata cheti za kuzaliwa.




Kaimu ofisa mtendaji wa Rita, Emmy Husdon 
Kaimu ofisa mtendaji wa Rita, Emmy Husdon  


Dar es Salaam. 
Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita) umesema kuanzia sasa Watanzania ni ruksa  kutumia Kitambulisho cha Taifa na kile cha kupiga kura kupata cheti cha kuzaliwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Februari 8, 2018 na kaimu ofisa mtendaji wa Rita, Emmy Husdon wakati akitoa taarifa kwa katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome aliyefanya ziara katika ofisi za Rita, jijini Dar es Salaam.
"Vyeti vya vizazi na vifo vinaweza kutolewa papo kwa hapo katika hospitali na vituo vya afya vilivyo katika majaribio,” amesema Husdon na kuongeza:
“Vituo hivyo ni pamoja na Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Temeke, Mbagala Rangitatu, Mbande Dispensary, Mnazi Mmoja, Kairuki na Hospitali ya Kinondoni.”
 Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...