Geita
Watumishi wanne wa
Serikali katika mikoa ya Mwanza na Geita wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za
kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita, imewaburuta mahakamani watumishi
wawili wa kitengo cha maabara katika Kituo cha Afya cha Uyovu kwa tuhuma za
kupokea rushwa.
Mwendesha mashtaka wa
Takukuru, Husna Kiboko ameieleza Mahakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo
Februari 2 kwa kupokea Sh25,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa kama
kishawishi cha kumpatia vifaa vya kutolea damu, kinyume na kifungu cha 15(1)
na kifungu cha pili cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11
ya mwaka 2007.
Husna amesema
washtakiwa hao pia walitenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
kinyume na kifungu cha 302 cha kanuni ya adhabu.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment