DAR ES SALAAM.
Tanzania inatarajiwa kufikisha idadi ya watu milioni
58 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la juu ikilinganishwa na
idadi ya awali ya watu milioni 46 iliyoripotiwa mwaka 2010.
Kwa mujibu wa Idara
ya Jamii na Mambo ya Uchumi ya Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), makadirio hayo
ni sawa na kila kilomita moja ya mraba kuna wakazi 67 tofauti na makadirio ya
mwaka 2010 ya watu 52.
Makadirio hayo pia
yanaonyesha kuwa idadi ya watu nchini imeongezeka kwa asilimia 3.15 kwa kipindi
cha miaka minane iliyopita wakati kiwango cha kuzaliana kilikuwa ni asilimia
5.17 kati ya mwaka 2015 na 2018.
Idadi ya hivi sasa ya
watu waishio mijini inakadiriwa kufikia milioni 19.2 sawa na asilimia 31 ya
idadi ya watu wote ikilinganishwa na ile ya awali ya mwaka 2010 iliyokuwa
milioni 12.6 ambayo ilikuwa sawa na asilimia 27.4.
Hata hivyo, kulingana
na makadirio ya idadi ya watu nchini mwaka 2016-17 yaliyofanywa na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS), ilikadiriwa kwamba kungekuwa na idadi ya watu milioni
51.55 katika kipindi cha mwaka jana.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment