Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi
DODOMA.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amekiri kuwapo kwa migogoro wa ardhi kati ya
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na wananchi eneo la Kisakasaka.
Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo
bungeni wakati akijibu swali la mbunge wa Dimani (CCM), Juma Ali Jumanne
aliyetaka kujua lini Serikali itaupatia ufumbuzi mgogoro huo.
Amesema katika kupatia ufumbuzi
wa mgogoro huu, Makao Makuu ya JWTZ imeridhia kurekebisha mpaka wa Kambi ya
Kisakasaka ili kuwaachia wananchi eneo lenye mgogoro.
Dk Mwinyi amewasihi wananchi kuwa
wavumilivu wakati Serikali inachukua hatua stahiki ili kuzuia madhara yoyote
yanayoweza kutokea kwa wananchi iwapo wataendelea na shughuli za kilimo na
mifugo katika eneo hilo.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment