TANGANYIKA
Wananchi wilayani Tanganyika wakipata huduma ya maji
Halmashauri ya Mpanda mkoa wa Katavi inakadilia kuwa ifikapo mwaka
2020 vijiji vingi vitafikiwa na maji safi na salama Wilayani Tanganyika kwa
asilimia 80.
Mhandisi wa maji Alkam Omary Sabuni amebainisha hayo mapema leo
kupitia Mpanda radio na kuitaja shabaha ya serikali kuwa nikuhakikisha sera ya
upatikanaji wa maji vijijini umbali wa mita 400 inatekelezeka kwa vitendo.
Katika hatua nyingine ameitaja baadhi ya miradi ya maji ambayo
inatumika na wananchi kama sehemu ya mikakati ya halmashauri hiyo kuwa ni mradi
wa maji Majalila, Igagala, Ikola na Mishamo.
Wiki hii benki ya dunia
imekubali kuisaidia Tanzania kiasi cha dola milioni 300 kwa
ajili ya ujenzi wa miradi ya maji safi
mijini na vijijini.
Chanzo: Allinanuswe
No comments:
Post a Comment