KATAVI
Jumuiya
ya wafanyabiashara Tanzania mkoani Katavi imethibitisha kurejeshwa kwa fedha za
wafanyabiashara waliokuwa wakidai kutapeliwa na baadhi ya makampuni yanayouza
mashine za kielektronic (EFDs) hapa nchini
Hatu
hiyo imethibitishwa na Katibu wa jumuiya hiyo Bw.Robison Thompson Bumela wakati
akizungumza na Mpanda Radio kuhusu hatima ya malalamiko ya wafanyabiasahara
waliokuwa wakidai kutapeliwa fedha bila kupata mashine hizo.
Aidha
katibu huyo amesema wafanyabiashara ambao bado hawajarudishiwa fedha zao ni
waliokuwa wamelipa bila kupewa risiti kutoka kwa wakala aliyekuwa akilalamikiwa.
Kwa
nyakati tofauti,Mkuu wa Mkoa wa Katavi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda
walikuwa wakiiagiza mamlaka ya ya Mpato Tanzania TRA kuhakikisha
wafanyabiashara wanapata fedha au mashine zao
Kwa
mjibu wa Bw.Bumela jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2014 ina wafanyabisahara
wanachama zaidi ya 150 na wafanyabiasahara waliokuwa wametapeliwa ni zaidi ya
kumi.
Chanzo:Isack Gerald
No comments:
Post a Comment