MPANDA
Wamiliki wa magari Mkoani Katavi wameaswa kutunza kumbukumbu za madereva
wanaowakabidhi magari wanayomiliki kwa mujibu wa kanuni ya 79 ya sheria ya
usalama barabarani.
Askari wa Jeshi la polisi kitengo cha usalama Barabarani Wilayani Mpanda PC Samwel Shigela amesema ni kosa
kwa mmliki kushindwa kutunza kumbukumbu hizo
.
PC Shigela amesema
ni wajibu wa wamiliki kuwatambua vizuri madereva wao ikiwa ni pamoja na
kuwapatia vitambulisho vya kazi
Kwa mujibu sheria ya
usalama barabarani sura ya 168
iliyofanyiwa maerekebisho mwaka 2002 kifungu cha 95 kimeainisha tozo kwa makosa ya papo kwa hapo kwa magari na pikipiki kuwa ni
Tsh 30000 kwa kila kosa
Chanzo :Ester Baraka
No comments:
Post a Comment