Tuesday, 20 March 2018

ULINZI SHIRIKISHI WAPUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU NSIMBO


NSIMBO


Wananchi katika Kijiji cha Sitalike Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi kwa kushirikiana na Viongozi wao wamesema wamefanikiwa kukomesha matukio mbalimbali ya kihalifu

Hatua hiyo imethibitishwa na mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw.Christopher Angelo Mrisho wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mikakati waliyonayo katika kupambana na uharifu kijijini hapo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Ilangasika kata ya Sitalike Bw.Michael Augustino Hamis pamoja na mambo mengine ameishauri serikali kutafuta fursa za ajira kwa vijana kwani uharifu unaotokea kwa kiasi kikubwa unahusisha vijana wasiokuwa na kazi maalumu za kufanya.

Kijiji cha Sitalike kipo kata ya Sitalike Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo ambapo halmashauri hiyo hivi karibuni imekumbwa na matukio ya watu wake kuvamiwa,kujeruhiwa,kuuwawa na uporaji wa mali.

Matukio ya hivi karibuni ni pamoja na tukio la uvamizi kata ya Ugalla na Mgodi wa Isulamilomo ambapo katika matukio hayo watu wawili waliuawawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Chanzo:Isack Gerald 


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...