MPANDA
Watumiaji wa vyombo vya moto katika Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi
wamelalamikia bei elekezi ya mafuta ya dizeli, mafuta ya taa na petrol
iliyotolewa na mamlaka ya uthibiti wa
maji na nishati Ewura.
Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kwa nyakati tofauti wamesema bei ya shilingi elfu 2400 kwa lita
imekuwa ngumu kuendesha shughuli kutokana na wateja wao kutoelewa mabadiliko ya
bei hizo.
Aidha wameziomba mamlaka zinazo husika ziwasaidie
kuliangalia suala hilo kwakina ilikurahisisha kazi zao kwani imekuwa vigumu
kufanya kazi hiyo kutokana na bei hiyo ambayo haiwapatii masilahi
Mapema mwezi huu mamlaka ya udhibiti wa maji na
nishati eura imetoa bei elekezi ya mafuta ya disel petrol na mafuta ya taa bei
ambayo ilionekana kuwa ya kiwango cha juu
Chanzo:Paul Mathius
No comments:
Post a Comment