KATAVI
Pundamilia katika hifadhi ya Taifa ya Katavi
Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi
Wananchi mkoani Katavi
wameshauriwa kujiwekea mazoea ya kutembea hifadhi ili kujifunza mambo
mbalimbali ikiwemo kukuza utali wa ndani
Hayo yamesemwa na muhifadhi wa mbuga ya mkoa wa Katavi KANAPA Athony Shirima wakati akizungumza na Mpanda radio na kusema kuwa hifadhi hiyo imetoa
fursa ya wananchi kujitokeza ili waweze kupata kuona vivutio vya mkoa wa katavi
pamoja nakupata elimu.
Aidha shirima amesema kuwa swala la ujangili limepungua kwa wingi
katika mbuga hiyo hali inayopelekea kuwepo kwa wanyama wengi wa aina tofauti
tofauti .
Pia amewataka wawindaji wanaowinda wanyama kinyume na taratibu za
hifadhi hiyo kuacha mara moja .
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment