MPANDA
PICHA YA CHOO BORA
Wananchi wa kijiji cha magamba Halimashauri ya Manspaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu juu ya
matumizi ya vyoo bora ili kuzuia magonjwa ya mlipuko.
Wakizungumza na mpanda radio kwa nyakati
tofauti wamesema hali ya matumizi ya vyoo bora katika kijiji hicho bado
hairidhishi huku wakieleza sababu ni ukosefu wa elimu na uhaba wa maji katika
eneo hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Magamba
Anna Thomas Mapazi amekiri kuwa baadhi ya wananchi hawana uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya
vyoo bora na kutoa wito kwa wananchi kujenga vyoo bora ili kulinda afya zao
dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
Asilimia 60 ya
kaya nchini hazina vyoo bora na
Kaya zenye vifaa maalum kama sabuni na
maji ya kunawa mikono ni 34% pekee.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment