KATAVI
KAMANDA WA POLISI MKOANI KATAVI ACP DAMAS NYANDA
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za
kuhamasisha maandamano kwa njia ya Mtandaoni.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP
Damas Nyanda wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu namna ambavyo jeshi hilo
limejipanga kudhibiti maandamano hayo.
Aidha Kamanda Nyanda ametoa onyo kali kwa watu watakaohamasisha au
kuandamana ambapo amesema watakaoandamana watakabiliwa na hatua kali za
kisheria.
Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi ambao wamezungumza na Mpanda Radio wakiwemo
Said Rashid,Juma Bairon,Jonathan Midende na Wenseslaus Obed wamesema maandamano
hayo hayana tija na hawatashiriki kwa sababu ya madhara yanayoweza kujitokeza.
Maandamano hayo yanayodaiwa kupangwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu
Chanzo: Issack Gerlad
No comments:
Post a Comment