Mkuu wa wilaya ya Tangayika Mh. Salehe Muhando akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga. |
KATAVI
Zaidi ya Shilingi milioni 152 zimechangwa na wadau wa
elimu wilayani Tanganyika,ili kutatua matatizo ya miundombinu ya elimu wilayani
humo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael
Muhaga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imefanyika Mpanda
Mjini,ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na serikali ili kuleta
maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tangayika Salehe
Muhando pamoja na mambo mengine amesema michango yote iliyopatikana lazima itumike
kwa malengo yaliyokusudiwa.
Naye Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Mh. Suleima
Kakoso baada ya kuchangia kompyuta kwa shule za sekondari,vifaa vya ujenzi na
fedha taslimu,amezishauri halmashauri Mkoani Katavi kuwashirikisha wadau wa
maendeleo walioko ndani na nje ya halmashauri zao ili washiriki kuleta
maendeleo.
Wadau wa elimu ambao wameshiki wanatoka taasisi za
kifedha,wafanyabiashara,madiwani halmashauri ya wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara
wilayani Tanganyika,wakulima, pamoja na watu binafsi.
Souce:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment