Diwani wa Kata ya Mwamkulu Kalipi Katani amesema kata yake ipo katika hatari
kubwa ya kimundombinu kutokana na barabara inayounganisha kata hiyo na maeneo
mengine kuzongwa na mafuriko.
Akizungumza na Mpanda Radio Katani amesema adha hiyo
imetokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kwamba sasa wananchi wanaendelea
kuathirika na hali hiyo.
Katika hatua nyingine amesema baadhi ya makazi yameharibiwa
na watu wawili wamepata majeraha baada ya kuangukiwa na nyumba.
Hata hivyo ameiomba mamlaka ya wakala wa barabara za mijini
na vijijini TARURA Kuchukua Hatu za matengenezo ya barabara hiyo.
Kata Ya Mwamkulu ni miongoni mwa kata zinzoongoza kwa
uzalishaji wa mpunga mkoani Katavi
No comments:
Post a Comment